SIMULIZI: Utamu Wa Shemeji Sehemu Ya Kwanza (1)

Ni asubuhi na mapema kijana Japhet akiwa amejilaza kitandani chumbani kwake ndipo mara ghafla anashtuka kutoka usingizini baada ya kuusikia mlango wa chumba alicholala ukigongwa. Kwa uchovu mwingi sana Japhet anaamka na kujiinua kutoka kitandani anachukua T-shirt yake na kuivaa vyema halafu anaenda kuufungua mlango huo. Kumbe ni kaka yake aitwae Lukasi ndie alikuwa anamgongea mlango. "Habari za asubuhi mdogo wangu, vipi umeamkaje?" Lukasi alimuuliza Japhet. "Habari za asubuhi ni nzuri tu kaka, nashukuru nimeamka salama" Japhet alijibu huku akipiga miayo ya uchovu. "Ok ni vizuri kama umeamka salama, sasa ni hivi mimi ndio naondoka ile safari yangu ya kibiashara, naenda Mwanza" alisema Lukasi akimwambia Japhet. "Ooho kaka mimi nakutakia safari njema uende salama na pia urudi salama hapa nyumbani" alisema kijana Japhet. "Sawa mdogo wangu, na nyinyi pia m'baki salama hapa nyumbani kumbuka ni wewe mdogo wangu ndie ninaekutegemea hapa muishi ...